Bidhaa

Mazao yenye ubora ujiuza. Wakulima ambao wanazalisha mazao bora hawaitaji kupata soko. Soko huja kwa ubora na hulipa ipasavyo. Hii ndio sababu tunadumisha viwango vya juu zaidi vya kimataifa kwa maendeleo ya nchi yetu. Sera yetu ni kuwahudumia wakulima wetu na bidhaa bora zaidi. Tunaweza kutoa aina kama: Mshare, FHIA-23, Nshakara, Mzuzu, Malindi, Matoke, Grand Naine, Cavendish, African Highlander, n.k.

Mchakato mzima wa utamaduni wa tishu kutoka meristem hadi miche huchukua karibu miezi 9-10. Kwa hivyo, ingawa ni wakati mfupi kuliko njia za kawaida, ikiwa unataka kuagiza miche yako ya ndizi kwa idadi kubwa, unahitaji kuzingatia mda.

Wasiliana nasi na kwa pamoja tutakua na suluhisho la mbegu bora za kutosha, kwa mahitaji yako. Kuagiza ni haraka na rahisi.

Pia tuna miche mingine kutokana na maitaji yako.

Unaweza pia kuagiza miche tofauti kutoka kwetu, kama: embe, parachichi, machungwa, mapera, papai, nyanya, mananasi, viazi na muhogo. Tuko wazi kuongeza matunda na mimea mipya kwa ombi lako.

Huduma zetu

Wataalam wetu wa kilimo wako tayari kukusaidia kuanza ukuzaji wa miche yako ya kitamaduni. Tunaweza kukusaidia na:

  • Upimaji wa udongo na uchambuzi
  • Mpango wa kuzalisha (kulingana na matokeo ya vipimo vya udongo)
  •  Programu ya Usafi