Msaada wa kijiditali

Wataalam wetu wanapatikana ili kukusaidia kuanzia kupanda hadi mavuno. Kilimo ni mchakato wa nguvu na kina wigo mpana. Wazo moja aliwezi kutatua changamoto zote, hata hivyo, kwa ufahamu wa udongo wako, maji na hali ya hewa tunaweza kukushauri juu ya mbolea, usimamizi wa migomba na mawazo ili kuzuia kuhatarisha uwekezaji wako.

Wakulima wanaowekeza katika ekari tano au zaidi ya ndizi wanapewa idhini ya kujiunga katika kikundi chetu cha kipekee cha kilimo Bora cha Ndizi WhatsApp. Hapa unaweza kushiriki kwa kuuliza maswali, kuweka picha ya miche yako na upate majibu mara moja kutoka kwa wataalam wetu wa ndizi. Tunataka kuwa sehemu ya safari ya wateja wetu, kutoka miche hadi shamba linalostawi.

Kuwa sehemu ya mfumo wetu wa msaada wa dijitali kunaweka msingi wa ufikiaji wa soko wenye nguvu pia. Wakati soko la ndizi la Tanzania ni kubwa, ni muhimu ujue ni nani wa kumuuzia na ni bei zipi zinapatikana. Kwa kuongezea, tunapokuza biashara zetu za ndizi pamoja, tunaweza kuandaa Tanzania kuwa taifa linalosafirisha ndizi nje. Fursa ni kubwa katika sekta hii, na teknolojia ya dijitali inachukua sehemu muhimu.

Mafunzo

 Mara nyingi, ni bora kuja kukutana na mtu, kupeana mikono na kupata uzoefu na uwekezaji wako wa miche. Hii ndio sababu tunatoa mafunzo ya bure na siku za maonyesho katika Kituo chetu cha Mafunzo, dakika 50, tuko kusini mwa Moshi, kwenye vitalu na mashamba yetu.

Kwa kibinafsi au katika mafunzo ya kampuni, yaliyotayalishwa kwa  mahitaji yako, yanaweza kupangwa kupitia wafanyakazi wetu wa mauzo. Walakini, hizi sio bure.

Pamoja na mwekezaji mwenzetu Rijk Zwaan tunaandaa siku za kuwa shambani ambapo mafunzo aina nyingi za mbegu zimepandwa ivi karibuni. Hii inatuweka mstari wa mbele katika maendeleo mapya katika ulimwengu wa kupanda mimea. Shughuli zetu zilizolengwa, kulingana na utumiaji wa mbinu za kisasa zinahitaji kuunganishwa na  ujuzi mkubwa kutoka kwa wataaramu wetu.